Video: Diamond na Swizz Beatz wakutana na kuzungumza New York

Producer huyo mkongwe, amewahi kupost video akifurahia nyimbo za wasanii wachache wa bara hili akiwemo Diamond. Na sasa wawili hao wamekutana jijini New York, Marekani.

Staa huyo wa ‘Kidogo’ yupo nchini humo alikoenda kutumbuiza kwenye tamasha la One Africa Music na Swizz alihudhuria. Swizz alipata muda wa kwenda kusalimiana na Diamond backstage.

Kwenye video zilizowekwa Instagram na Snapchat, Diamond anaonekana akimtambulisha Swizz kwa timu yake akiwemo Babutale, Dj D-Ommy na mtangazaji wa Clouds FM, B12 ambaye baadaye alimhoji.

Tazama video hiyo chini.


Comments

Popular posts from this blog

NINI MAANA KIGOLI?. AU BINTI KIGOLI

Mambo 10, ya kumfanya mpenzi wako akupende milele@ Kama uliamini mapenzi pesa... SAHAU