M-PESA ya Vodacom sasa kupatikana katika teknojia mpya ya G2

Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania leo imetangaza kubadilisha huduma yake ya fedha ya M-Pesa kutoka teknolojia ya awali ya G1 kwenda mpya ya G2, lengo kubwa ikiwa ni kuboresha huduma hii kwa kuiingiza katika teknolojia ya juu ili iweze kupatikana wakati wowote kwa uhakika na kwa kasi kubwa wakati wa ufanyaji wa mihamala ya malipo na huduma mbalimbali.
002
Afisa Mkuu wa Idara ya huduma kwa wateja wa Vodacom Tanzania,Harriet Lwakatare(kushoto)na Mkurugenzi Mkuu wa Huawei,Bruce Yang(katikati)wakimsikiliza jambo Mkurugenzi Mtendaji wa Financial Sector Deepening Trust(FSDT) Sosthenes Kewe(kushoto) wakati wa hafla ya uzinduzi wa teknolojia mpya ya huduma ya M-Pesa ya G2 mwishoni mwa wiki itakayo kuwa ikipatikana wakati wowote kwa uhakika na kwa kasi kubwa wakati wa ufanya mihamala ya malipo na huduma mbalimbali
Matumizi ya teknolojia mpya ya G2 ambayo miundombinu yake imejengwa hapa nchini itarahisisha matengenezo yake pindi yatakapojitokeza matatizo ya kimtandao pia itawezesha kupanuka kwa matumizi ya huduma hii kwenye kuboresha na kuunganisha huduma mbalimbali na kibiashara.
001
Mkurugenzi Mtendaji wa Financial Sector Deepening Trust(FSDT) Sosthenes Kewe(kushoto)akibadilishana mawazo na Afisa Mkuu wa biashara Idara ya M-Pesa wa Vodacom Tanzania,Sitoyo Lopokoiyit,wakati wa hafla ya uzinduzi wa teknolojia mpya ya huduma ya M-Pesa ya G2 mwishoni mwa wiki itakayo kuwa ikipatikana wakati wowote kwa uhakika na kwa kasi kubwa wakati wa ufanya mihamala ya malipo na huduma mbalimbali.Katikati ni Mkuu wa kitengo cha teknolojia za kisasa wa kampuni ya(FSDT) Innocent Ephraim
Akiongea wakati wa uzinduzi wa matumizi ya teknolojia hii mpya katika hafla iliofanyika leo,Afisa Mtendaji Mkuu wa huduma za malipo ya mtandao wa Vodacom Tanzania, Sitoyo Lopokoiyit amesema, “Tunawaletea huduma ya M-pesa katika teknolojia mpya na bora zaidi,tunajivunia kwa kazi nzuri iliyofanyika kufanikisha mabadiliko haya ambayo yatawawezesha watanzania kupata huduma bora za kifedha kupitia huduma ya M-Pesa iliyoboreshwa zaidi.Ubunifu na matumizi ya teknolojia hii mpya yataboresha huduma hii sio kwa wateja wa Vodacom pekee bali biashara mbalimbali na huduma zinazofanyika kupitia huduma hii.”
003
Mkurugenzi Mkuu wa Huawei,Bruce Yang(kushoto)akisalimiana na Afisa Mkuu wa biashara Idara ya M-Pesa wa Vodacom Tanzania,Sitoyo Lopokoiyit,wakati wa hafla ya uzinduzi wa teknolojia mpya ya huduma ya M-Pesa ya G2 mwishoni mwa wiki itakayo kuwa ikipatikana wakati wowote kwa uhakika na kwa kasi kubwa wakati wa ufanya mihamala ya malipo na huduma mbalimbali.Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Financial Sector Deepening Trust(FSDT) Sosthenes Kewe
Sitoyo aliongeza kusema kuwa teknolojia hii italeta mapinduzi makubwa ya matumizi ya huduma za kifedha kwa njia ya mtandao wa simu na Vodacom itaendelea kujenga mazingira ya kukuza biashara za malipo kwa njia ya mitandao na kuzidi kuiweka Tanzania mbele katika huduma za biashara kwa njia ya mtandao pia kuongeza wigo wa huduma za kimtandao kama vile kuweka akiba,kuchukua na kulipa mikopo,ufanyaji wa mihamala ya malipo kwa mtandao,huduma za bima na huduma nyinginezo nyingi tofauti na ilivyokuwa hapo awali.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Huawei,Bruce Yang alisema, “Kupitia teknolojia ya kiwango cha juu ya Huawei,Huduma za M-Pesa zimebadilika kabisa na kuwa za kiwango kikubwa cha ubora na imeboreshwa zaidi kuweza kukidhi matakwa ya huduma mbalimbali za kifedha.Kwa kutumia timu ya wataalamu wetu tumeweza kujenga miundombinu ya kisasa itakayowawezesha watanzania kupata huduma za kifedha kwa viwango vya kimataifa.Tumefurahishwa na ushirikiano tulioupata kutoka timu nzima ya wafanyakazi wa Vodacom hali iliyotuwezesha kumaliza mradi huu wa kubadilisha teknolojia mapema tofauti na jinsi tulivyotegemea.”
004
Kutoka kushoto Mkurugenzi Mtendaji wa Financial Sector Deepening Trust(FSDT) Sosthenes Kewe, Afisa Mkuu wa Idara ya huduma kwa wateja wa Vodacom Tanzania,Harriet Lwakatare,Mshereheshaji wa hafla,Taji Liundi, Mkurugenzi Mkuu wa Huawei,Bruce Yang,Mkuu wa kitengo cha M-Pesa wa Candice Rato,wakibonyeza kitufe cha kompyuta ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa teknolojia mpya ya huduma ya M-Pesa ya G2 mwishoni mwa wiki itakayo kuwa ikipatikana wakati wowote kwa uhakika na kwa kasi kubwa wakati wa ufanya mihamala ya malipo na huduma mbalimbali
Huduma ya M-Pesa ya Vodacom Tanzania ikiwa ni ya kwanza kwa kutuma , kupokea fedha na kufanya mihamala mbalimbali ya malipo inaaminika kwa watanzania wengi.Tangia ianzishwe katika kipindi cha miaka 8 iliyopita inao watumiaji wapatao milioni 9.Kupitia teknolojia hii mpya ya G2,huduma za M-Pesa zimeboreshwa kuwa nzuri na ubunifu wa kutumiwa kwa malipo, huduma mbalimbali na kuwa na uwezo wa kuunganisha biashara.
005
Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania,wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa teknolojia mpya ya huduma ya M-Pesa ya G2 mwishoni mwa wiki itakayo kuwa ikipatikana wakati wowote kwa uhakika na kwa kasi kubwa wakati wa ufanya mihamala ya malipo na huduma mbalimbali mwishoni mwa wiki
Mabadiliko haya ni ya kihistoria katika huduma za kifedha kwa njia ya simu nchini Tanzania na kampuni inawahaidi watumiaji wategemee ubunifu wa kila aina kwa matumizi ya huduma hii katika teknolojia hii ambayo kuanza kwake kutumika nchini ni mafanikio makubwa katika kuboresha huduma za kifedha kwa watanzania . Vodacom Tanzania inajivunia kufanikisha kuleta teknolojia hii ambayo inategemewa kuleta mapinduzi makubwa ya huduma za kifedha nchini

Comments

Popular posts from this blog

NINI MAANA KIGOLI?. AU BINTI KIGOLI

Mambo 10, ya kumfanya mpenzi wako akupende milele@ Kama uliamini mapenzi pesa... SAHAU