Majaliwa: Nahamia rasmi Dodoma Septemba
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema atahamia rasmi Dodoma mwezi Septemba mwaka huu.
Akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Kumbukumbuku ya Siku ya Mashujaa Majaliwa ameagiza mawaziri wote wanahamie Dodoma kutekeleza tamko la Rais John Magafuli la serikali anayoingoza kuhamia Dodoma kabla ya kumaliza kipindi chake cha miaka mitano.
''Wanadodoma nawahakikishia ifikapo Septemba nahamia pale juu. Kama ofisi zote za serikali zinahamia hapa, ni wazi wageni nao watakuwa wanakuja Dodoma", alisema Majaliwa.
Mapema Rais Magufuli alisisitiza tamko lake alilotoa wakati wa kukabidhiwa uenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) kuhamia Dodoma akisema hakuna sababu ya serikali kukwama kutekeleza mpango huo.
Aidha Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, Rais wa Zanzibar, Ali Mohamed Shein na Waziri Mkuu Mstaafu John Malecela wamesisitiza wananchi wa Tanzania kumuunga mkono Rais katika mpango wake wa kuhakikisha serikali inahamia Dodoma.
Wamesema kufanikiwa kwa mpango huo si tu kuna manufaa kwa wananchi wa Dodoma bali pia Tanzania nzima
Comments
Post a Comment