Diamond athibitisha kuja na collabo na Swizz Beatz

Collabo kati ya Diamond Platnumz na producer na rapper mkongwe wa Marekani, Swizz Beatz inakuja.
Diamond
Staa huyo amethibitisha kuwa alizungumza na Beatz kuhusu kufanya wimbo wao walipokutana New York kwenye tamasha la One Africa Music.
“Tulikuwa tunazungumza kuhusu project ambayo tunatakiwa tuifanye, tuifanye Tanzania au tuifanye wapi, tulikuwa tunaangalia kwa benefit zote pia,” Diamond aliiambia 255 ya kipindi cha XXL kupitia Clouds FM.
“Mimi nilichosuggest nilimuambia ni vizuri tukifanya lakini tuwe na producer wa Afrika kumix vitu vya Kiafrika na tunaweza tukaifanyia huku tukatoka nayo tukaenda kuifanyia Tanzania pia sababu itaongeza impact kwa Afrika na kuonesha wamarekani kweli wanania ya kusaidia muziki wa Afrika,” aliongeza.
Tayari Diamond amesharekodi collabo nyingine na msanii wa Marekani, Ne-Yo

Comments

Popular posts from this blog

NINI MAANA KIGOLI?. AU BINTI KIGOLI

Mambo 10, ya kumfanya mpenzi wako akupende milele@ Kama uliamini mapenzi pesa... SAHAU