Makonda Awawashia Moto Wakurugenzi
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewabadilikia Wakurugenzi mbalimbali wa halmashauri za wilaya mbalimbali jijini Dar es Salaam kwa vitendo vyao vya kuwakaiimisha nafasi mbalimbali viongozi ambao hawana uwezo.
Makonda amesema hayo leo Februari 10,2018 alipokutana na wananchi wa Mkoa wa Dar es salaam ili kujibu kero na matatizo mbalimbali yanayowakabili ikiwa ni siku ya mwisho kwa zoezi la kupokea na kuzitafutia ufumbuzi kero hizo. Katika kusikiliza kero hizo baadhi ya watendaji wa Serikali walikuwa wakishindwa kujibu maswali ambayo Mkuu wa Mkoa alikuwa akiwauliza.
"Mkurugenzi huyu mmempaje nafasi ya kukaimu, kwa hiyo Mkuu wa Idara anampa mtu ambaye hana uwezo kukaimu idara ili asipate idara si ndiyo maana yake? Maana huyu ndani tunatabia moja Mkuu wa Idara hana uwezo sasa hivyo anampa nafasi mtu ambaye hana uwezo ili yule mwenye uwezo asionekane, sasa huyu hana majibu anafanya nini hapa? Hajui lolote wala hana ripoti yoyote sasa Kukaimu kwake kumeishia kwenye huu Mkutano tafuteni mtu mwingine akakaimu"
"Halafu nyinyi Wakurugenzi nisaidieni mnawapaje watu idara wasiokuwa na uwezo, yaani anaitwaje Mkuu wa Idara hakuna jambo linalonifedhehesha kuona wananchi wanapata shida, Mkuu wa idara anaulizwa kwenye eneo lako kuna migororo mingapi ya ardhi anakwambia kwangu hakuna kabisa lakini anasimama Mwanasheria anasema migogoro ipo na tunahangaika kuitatua na Mkurugenzi sasa huyo ni Mkuu wa Idara kweli? Halafu mwisho wa siku kinatukanwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kumbe kwa uzembe wa mtu mmoja aliyekaa kwenye kiti anakula mshahara wa wananchi bila kufanya kazi yake"

Comments
Post a Comment