Skip to main content

Cristiano Ronaldo hayumo hata kwenye 5 bora - Nani mchezaji bora Euro 2016?

Cristiano Ronaldo hayumo hata kwenye 5 bora - Nani mchezaji bora Euro 2016?






Nahodha huyo wa Ureno aliiongoza timu yake ya taifa kutwaa kombe la kwanza Ulaya, lakini alipata majeraha mechi yake ya mwisho na hayumo katika wachezaji bora
Nahodha huyo wa Ureno, ambaye mechi yake ya fainali alitolewa mapema kwa sababu ya majeraha yaliyomlazimu kupumzika kipindi cha kwanza, alikuwa mchezaji wa pili kwa kupachika mabao katika michuano lakini anashika nafasi ya saba katika viwango vya barometa nafasi moja sawa na Mbelgiji Eden Hazard.
Mfaransa Dimitri Payet  ametambulika kama mchezaji bora wa michuano.
Tangu Julai 3 Payet ameshikilia katika msimamo huo licha ya kushushwa kidogo na Antoine Griezmann ambaye ameibuka kuwa mshindi wa kiatu cha dhahabu.
Barometa ya wachezaji inathaminisha data mbali mbali kulingana na mchezaji na nafasi yake anayocheza hali kadhalika ufanisi wake dhidi ya wapinzani imara wanaokutana dimbani.
Nyota wa Wales, Gareth Bale anashika nafasi ya tatu baada ya kuiongoza timu yake kuweka historia ya kufika nusu fainali wakati kiungo wa Ujerumani Toni Kroos na Mbelgiji Kevin de Bruyne amemaliza ndani ya tano bora pia.
Ureno walizuka na kuifunga Ufaransa 1-0 katika mechi ya fainali ambayo Nani, Rui Patricio, Pepe na Raphael Guerreiro wote waliungana na nahodha wao kutinga 20 bora katika juma la mwisho la michuano

Comments

Popular posts from this blog

NINI MAANA KIGOLI?. AU BINTI KIGOLI

Mambo 10, ya kumfanya mpenzi wako akupende milele@ Kama uliamini mapenzi pesa... SAHAU