Barnaba kufanya haya baada ya kuboresha studio ya ‘High Table Sound
Msanii na mtayarishaji wa muziki wa ‘High Table Sound’ Barnaba Classic amesema baada ya kukamilisha maboresho ya studio yake, mashabiki pamoja na wadau wa muziki watarajie mambo mazuri kutoka kwake.
Akiongea na Bongo5 wiki hii, Barnaba amesema studio hiyo kwa sasa anaitumia kufanya finishing ya albamu yake mpya ‘Nane Nane’ ambayo itatoka mwezi ujao.
“Mashabiki watengemee mambo makubwa sana kutoka kwangu, sound kali, kwa sababu hali ya studio kwa sasa imeniongezea mzuka wa kufanya kazi, kwa hiyo ni mambo makubwa yanakuja,” alisema Barnaba.
Aliongeza, “Pia mashabiki wangu wakae mkao wa kula kwa ajili ya albamu ya ‘Nane Nane’, ni kali na kwa sababu ipo tayari sema nipo kwenye finishing,”
Comments
Post a Comment