Wataalamu: Vitamini nyingi haziwafai KWA wajawazito
Utathmini mpya wa wataalamu umedokeza kwamba tembe za vitamin mseto zinazopewa wajawazito huwa ni kupoteza pesa bure.
Kwa kawaida, wajawazito wamekuwa wakipewa tembe zenye aina ya vitamin hata zaidi ya 20 pamoja na madini mengine.
Matokeo ya utathmini huo yamechapishwa katika jarida la Drug and Therapeutics Bulletin, ambalo huwafahamisha madaktari na wauzaji dawa Uingereza kuhusu tiba na udhibiti wa maradhi.
Utafiti huo umegundua kwamba vitamini mseto huwa haziwawezeshi kina mama wajawazito na watoto wao kuwa na afya bora na kwamba ni “gharama isiyo na maana”.
Badala yake, wataalamu hao wanapendekeza kwamba wanawake wanafaa kuangazia zaidi kumeza au kunywa vitamin zilizo kivyake ambazo kwa mfano nchini Uingereza hupatikana kwa peni kadha.
Vitamini hizo, ambazo hupendekezwa na Shirika la Taifa la Afya Uingereza (NHS), ni vitamin B9 au kwa Kiingereza folic acid miezi ya tatu ya kwanza ya ujauzito, na vitamin D.
Wanafaa pia kula lishe bora na yenye afya.
Comments
Post a Comment