HAMISA Mobeto Ataka Kumuua Zari Kwa Presha...
Mrembo anayetikisa kwa sasa kwenye kizazi cha mitindo Bongo, Hamisa Hassan Mobeto, anadaiwa kutaka kumuua kwa presha mzazi mwenzake Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari’, kufuatia kuvuja kwa habari kwamba, amejibinafsisha penzi la nyota huyo, Amani limechimba.
Chanzo cha habari kimenyetisha kwa Amani hivi karibuni kwa kusema kwamba, nyumbani kwa Diamond, Madale jijini Dar hakuna amani hata kidogo kufuatia mtifuano mkali baina ya Zari na wifi yake (Esma) na mkwe wake (Sanura Kasim) ambapo kisa chote kinadaiwa kusababishwa na Mobeto ambapo wengi wanasema ni mpenzi mpya wa Diamond kwa sasa na kwamba, ndugu ndiyo wanamkubali kuliko ‘Mzungu’ Zari.
SIKIA CHANZO HIKI
“Ndugu yangu ngoja nikupe ubuyu uliyokwenda shule, hivi unafahamu amani ya mapenzi kati ya Zari na Diamond imekwisha kiasi cha kusababisha Zari kutowaelewa tena ndugu wa mzazi mwenzake huyo?
“Yaani ishu iko hivi; Zari alikuja pale Madale kujumuika katika bethidei ya mama Diamond (Alhamisi iliyopita), lakini inavyooneka alitonywa kwamba, Diamond siku hizi anatoka na Mobeto, presha juu mtoto wa watu.”
VIOJA KWENYE BETHIDEI
“Yaani kwenye hiyo sherehe sasa, tulishuhudia vioja vya kila aina kwani kulikuwa na vijembe vya kutosha kati ya Zari na Mobeto. Huwezi amini, Mobeto siku hiyo alikuwa ndiye mpendwa wa familia kwani Esma na mama yake walikuwa karibu naye kuliko Zari. Mtoto wa watu, amani ilitoweka.
“Kwa mtu yeyote ambaye alialikwa kwenye ile shughuli anajua mauzauza yaliyoendelea. Mobeto alikuwa kama ndiyo yuko kwenye shughuli yake ya kutolewa mahari. Jamani mapenzi nyie! Zari anajuta kuja Bongo, anatamani angeona picha kwenye mitandao tu,” kilisema chanzo hicho.zari
Zari
KEKI YA MAMA D IAMOND KWA MOBETO
Habari zaidi zinasema kuwa, upendo wa mama Diamond kwa Mobeto ulikuwa dhahiri kiasi kwamba, wakati wa kuwalisha keki waalikwa, alimlisha Mobeto kwa furaha kuliko Zari.
KEKI KWA MKONO WA KUSHOTO?
Kuna habari nyingine zinadai kwa-mba, wakati wa Zari kulishwa keki, mama Diamond alitumia mkono wa kushoto hali iliyowashangaza wengi na kuhoji kulikoni licha ya kwamba, mikono yote ipo kwenye mwili mmoja na Muumba ni mmoja.
MUDA MWINGI ZARI PEKE YAKE
Amani ambalo lilipata bahati ya kunyetishiwa hayo na mmoja wa wahudhuriaji, alizidi kusema kuwa, muda mwingi Zari alikuwa peke yake, akiongezeka mtu ni mwanaye, Latifa ‘Tifah’ huku, mama mkwe wake, wifi yake na Mobeto wakisakata nyimbo za taarab ambazo kama ni DJ ndiye aliyeweka ‘playlist’ (mpangilio wa kupigwa) basi aliambiwa kwani nyingi zilikuwa kijembe cha wazi kwa Zari na timu yake.
AMANI LAMTAFUTA MOBETO
Juzi baada ya kuzinyaka habari hizo, Gazeti la Amani lilimtafuta Mobeto kwa lengo la kumpa nafasi ya kuzungumzia madai hayo lakini baada ya kupatikana aligoma kuongelea chochote juu ya sakata hilo na kuishia kusema haoni sababu kwani asingependa kuendelea kuwapa watu muda wa kuzungumzia mambo yake.
“Kusema kweli hapo sina cha kuongea wala nisingependa kuongelea ishu hizo. Sina lolote la kusema hapo na nisingependa kuwapa watu maneno ya kusema, yaani kwa kifupi sina comments zozote,” alisema Mobeto.
HUYU HAPA DIAMOND
Kwa upande wake, Diamond baada ya kutafutwa ili azungumzie sakata hilo naye aligoma huku akisema kuwa, hayo ni mambo yaliyomo kwenye mitandao hivyo hana cha kuongeza.
“Kwa hili sina la kuongelea maana ni habari nisizozielewa hivyo nisingependa sana na mimi kushiriki, yaani kwa kifupi sina cha kuongea juu ya hilo maana zinaniweka katika hali mbaya. Wakati ukifika nitasema,” alisema Diamond.
Mama Diamond hakupatikana hewani kuzungumzia madai hayo kwani simu yake juzi Jumanne ilikuwa ikiita bila kupokelewa.
GLOBAL NA BETHIDEI
Bethidei zote za mama Diamond, Global wamekuwa wakialikwa lakini ya safari hii, ilibidi Global itumie mbinu zake kupata ubuyu kwani kuna habari kwamba, uongozi wa Wasafi Classic Baby (WCB) umezuia kwa kuhofia siri nyingi za ndani ya shughuli hiyo kujulikana na wengi licha ya waalikwa wengi kuingia wakiwa ni marafiki wa Global (kichekesho)!
Chanzo: GLOBAL

Comments
Post a Comment