Kifaa cha Kurekodi
Ukiona kifaa hiki kwenye chumba cha hotel, ujue kwamba sio urembo kama watu wengi wanavyofikiria. Kifaa hiki unaweza kuona kimewekwa kwenye mlango au ukutani. Kinawekwa na waharifu kwa manufaa yao binafsi.

Habari mpya na zenye matumaini zinaeleza kwamba hiki kifaa chenye umbo kama pasi, kinabeba kitu ambacho kinaweza kuharibu maisha yako.Usikubali watu hawa wapate wanachotaka kwako.Vingi kati ya vifaa hizi ni technolojia ya juu sana ya kamera za siri.

Cha kusikitisha zaidi kuhusu hizi kamera ni kwamba mtu yeyote anaweza akazinunua kwenye mtandao. Ina maana kwamba mtu yeyote akidhamilia kukuchunguza ataweza, ni fedha chache tu inagharimu kwa mtu kupata hiki kifaa.

Vifaa hivi vinatangazwa kama "home security camera". Ila kwa bahati mbaya watu wengi wanavinunua kuwachunguza wanawake katika vyumba vya kulala wageni na vyumba vya hotelini.
Nchini Marekani vifaa hivi vimeanza kuchunguzwa kwenye vyumba vya wageni. Polisi wengi wanahusika na uchunguzi wa vifaa hivi, kama utakiona katika sehemu unayopendelea kwenda, inabidi ujiulize kwanini?

Unashauriwa ukikiona kifaa hiki chumba cha wageni ulicholala, au kifaa chochote usichokielewa vizuri ambacho utahisi kama ni kamera, usikishike.Wapigie polisi na wajulishe.
Kamera nyingi za siri zinapatikana kwenye maduka mbalimbali yanayouza vifaa hivi. Ukikiangalia kwa karibu utaona kitobo kidogo sana juu yake.Hiyo ni sehemu ya lenzi ya camera na inakurekodi kila kitu unachofanya.

Hizi kamera zinaenda kwa motion.Kama mtu akiingia tu bafuni, inajiwasha yenyewe.Itakurekodi ukiwa bafuni mpaka utoke au nafasi yake ijae.
Kuwa makini na kamera hizi, zinaweza kufichwa mahali popote na wewe usiweze kugundua kabisa

Comments

Popular posts from this blog

NINI MAANA KIGOLI?. AU BINTI KIGOLI

Mambo 10, ya kumfanya mpenzi wako akupende milele@ Kama uliamini mapenzi pesa... SAHAU