Msichana mweusi kuwa Iron Man
Kampuni ya vitabu vya vibonzo vya ucheshi ya Marvel imefichua kwamba msichana mweusi wa umri wa miaka 15 ndiye atakayeigiza Iron Man katika filamu ijayo ya mfululizo wa filamu hizo.
Katika filamu hiyo itakayoitwa Civil War II, mavazi ya Iron Man yatavaliwa na mhusika atakayeitwa Riri Williams.
Atachukua majukumu hayo kutoka kwa Tony Stark.
Mhusika Riri Williams ni mzaliwa wa Chicago ambaye ni gwiji wa sayansi na anasomea chuo cha MIT.
Mtunzi wa hadithi za Iron Man Brian Michael Bendis ameambia gazeti la Time kwamba alibuni mhusika Williams baada ya kuguswa na “visa vya ghasia, fujo na ukatili” ambavyo vilikuwa vinatokea Chicago alipokuwa anafanya kazi huko.
“Na simulizi hii ya mwanamke kijana, mwerevu ambaye maisha yake yamekumbwa na mikasa na hatari ambayo ingeangamiza maisha yake, ghasia mitaani, na alifanikiwa kwenda chuo ilinigusa sana,” amesema.
"Nilifikiri hiyo ni aina ya kisasa zaidi ya hadithi ya shujaa ambayo nimewahi kuisikia.”
Mhusika wa Iron Man alianza kutumiwa mara ya kwanza 1963.
Habari kwamba mhusika wa sasa atakuwa mwanamke na mweusi imesifiwa na wengi wanaoitazama kama hatua ya kukumbatia jinsia na watu wa asili mbalimbali
Comments
Post a Comment