Shilole: Huyu Ndiye Mrithi wa Nuh Mziwanda
Shilole na Mpenzi wake mpya |
Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni baada ya kubambwa kwenye Ukumbi wa King Solomon uliopo Namanga jijini Dar es Salaam ilipokuwa ikifanyika Shoo ya Black Tie, Shilole alisema ameamua kubadili upepo na kuachana na mapenzi ya vijanahivyo ameangukia kwa mwanaume huyo ambaye ni mtu wa rika lake.
“Kusema kweli leo sitaki hata kupaparika maana nimekuja na mheshimiwa hivyo sitaki tena kuonekana kama mtoto mdogo humu ukumbini, angalia hata meza niliyokaa utagundua kuwa hapa ishu zote ni za kiutu uzima, siwezi tena kupaparika, ifikie muda tuheshimiane kwani njia pekee ya kujiheshimu ni kutoka na watu wenye msimamo wao nawatu wazima kama huyu.
“Sipendi sana kumuelezea huyu mtu wala kumtambulisha kwa jamii kwani siyo vyema sana na hata ukiangalia jinsi tulivyokaa utagundua hatutaki kujionesha kwa watu, sitaki tena ishu za kuhangaika na watoto wadogo wasiojielewa kama huko nyuma nilivyokuwa nikihangaika,” alisema Shilole huku akigoma kumtaja jina mwanaume huyo na kusisitiza kuwa ndiye mwandani wake wa sasa.watu wazima kama huyu.
“Sipendi sana kumuelezea huyu mtu wala kumtambulisha kwa jamii kwani siyo vyema sana na hata ukiangalia jinsi tulivyokaa utagundua hatutaki kujionesha kwa watu, sitaki tena ishu za kuhangaika na watoto wadogo wasiojielewa kama huko nyuma nilivyokuwa nikihangaika,” alisema Shilole huku akigoma kumtaja jina mwanaume huyo na kusisitiza kuwa ndiye mwandani wake wa sasa.
Comments
Post a Comment