Lulu aeleza mapinduzi yanayoletwa na filamu yake mpya ‘Ni Noma’ inayotoka Ijumaa hii (Video)
Baada ya kimya cha muda mrefu, mshindi wa tuzo za Africa Magic, Elizabeth ‘Lulu’ Michael, anakuja na filamu yake mpya iitwayo ‘Ni Noma.’
Filamu hiyo inaingia sokoni Ijumaa hii kwa mfumo wa dijitali ambapo watu watainunua na kuingalia kwenye smartphone zao kupitia app ya Proin Box.
Lulu ameiambia Bongo5 kuwa filamu hiyo imekuja na mapinduzi makubwa kwa kila kitu kuanzia teknolojia na uigizaji. Amedai kuwa yeye na kampuni yake ya Proin, walitaka kuja na kitu tofauti na vilivyozoeleka kwenye filamu za Tanzania.
“Ilitubidi kwa kiasi fulani tutulie, tusome mazingira, tasnia yetu inamiss nini sasa hivi, mashabiki wetu wanahitaji nini sasa hivi,” anasema Lulu.
“Tumejitahidi kufanya production ya tofauti ambayo ina quality nzuri, it needs time, sio kama zamani kwa siku mnaweza mkashoot scene sita, saba, lakini saa zingine production kwa siku tulikuwa tunaweza kushoot scene mbili tu lakini mnahakikisha mnatoka na kitu kizuri,” ameongeza.
Amedai kuwa hata sauti zingine pia ilibidi waziingize upya studio ili kuwa na kitu bora kama ambavyo hufanyika kwenye filamu za Hollywood.
Lulu amesema watu wataweza kununua filamu hiyo kwenye app ya Proin Box kwa shilingi 2,500 tu kwa kupitia huduma za malipo ya simu kama M-Pesa, Airtel Money na zingine huku wale waliopo nje wakiweza kununua kwa credit cards.
Amesema baada ya kuizindua kwa mfumo wa dijitali, filamu hiyo itaanza kuoneshwa kwenye majumba ya sinema na kisha baadaye kuuzwa kwenye DVD. Hata hivyo ameeleza kuwa kwenye DVD hizo kutakuwa na vitu vya ziada kama vile behind the scenes, interview na vitu vingine.
Comments
Post a Comment