Utafiti: Farasi wanaweza kuwasiliana na binaadamu
Farasi wamejiunga na kundi la wanyama wanaoweza kuwasiliana kwa kuonyesha ishara.
Wanasayansi waliwapatia mafunzo farasi , kwa kuwazawadi vipande vya karoti, ili waguse ubao kwa pua zao kudhihirisha iwapo wanataka wavishwe blanketi.
ombi la farasi ha liliambatana na hali ya hewa, kuashiria kuwa sio ombi la hivi hivi tu.
Wanyama wengie wakiwmo nyani wanaonekana kama binaadamu wakijaribu kuwasiliana kwa kuashiria kueleka wanachokitaka.
Dr Cecilie Mejdell wa taasisi ya kutibu wanyama, aliyeongoza utafiti huo anasema walitaka kutafuta namna ya kuuuliza farazi iwapo anapnda au hapendi kuvaa blanketi.
Katika nchi za kaskazini mwa Ulaya, ni kawaida kwa farasi kuvaa blanketi wakati wa msimu wowote.
"Nadhani utafiti wetu unaongeza maarifa kuhusu namna ya kuwaelewa farasi - kuhusu wanachoweza kujifunza farasi na wanavyofikiria," ameiambia BBC.
Utafiti wote ulifanyika kwa zaidi ya wiki mbili kwa dakika 10 hadi 15 za mafunzo kila siku.
Wanasayansi wanatarajia kuwa watafiti wengine watatumia mbinu yao kuwauliza farasi maswali zaidi.
Na wanadhani wanaowafunza farasi kusiih na watu wataweza kutumia mbinu hii kuwasiliana nao.
Karen McComb, profesa anayejishughulisha na tabia z wanyama katika chuo kikuu cha Sussex, anasema mbinu hii yakutoa mafunzo huenda ikawa na faida katika kujali maslahi ya wanyama
"Inafurahisha kweli na ni utafiti uliovumbuwa njia nzuri wa kujua yanayoendelea katika akili ya farasi," alisema.
Wakati mawasiliano na paka na mbwa ndio yanayoangaziwa pakubwa katika utafiti, wanyama wengine wa nyumbani wanaonekana kusahauliwa.
Mapema mwaka huu, watafiti Uingereza walifanikiwa kutofautisha kati ya sura ya furaha na ya haisra ya mwanadamu.
Wanasayansi wanasema kufugwa farasi nyumbani huenda kumewasaidia kuelewa mienendo ya binaadamu
Comments
Post a Comment