PAPA FRANCIS akutana na Rais JOSEPH KABILA

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Baba Mtakatifu FRANCIS amekutana na Rais JOSEPH KABILA wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya CONGO
Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Baba Mtakatifu FRANCIS (kulia) na Rais JOSEPH KABILA
Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Baba Mtakatifu FRANCIS amekutana na Rais JOSEPH KABILA wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya CONGO na kumtaka kumaliza mapigano yaliyozuka kati ya majeshi ya serikali na ya upinzani kwa njia ya majadiliano.
        
Mapigano hayo yamezuka baada ya Tume ya Uchaguzi ya DRC kutangaza kuwa uchaguzi mkuu wa nchi hiyo hautafanyika Novemba mwaka huu kama ilivyopangwa kwa kuwa taratibu za uandikishaji kwenye daftari la wapiga kura zitakuwa hazijakamilika kwa wakati.

Kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo Rais aliyepo madarakani ataendelea kuongoza hadi pale uchaguzi utakapofanyika.

Baba Mtakatifu FRANCIS na waziri wa Mambo ya Nje wa VATICAN wamesisitiza viongozi wa kisiasa, kidini na wa vyama vya kiraia kuhakikisha amani inapatikana kwa njia ya majadiliano

Comments

Popular posts from this blog

NINI MAANA KIGOLI?. AU BINTI KIGOLI

Mambo 10, ya kumfanya mpenzi wako akupende milele@ Kama uliamini mapenzi pesa... SAHAU