Mtoto azaliwa kutoka kwa mbegu za watu 3

Teknolojia mpya ya uzazi ndio iliotumika kumtengeza mtoto huyo
Image captionTeknolojia mpya ya uzazi ndio iliotumika kumtengeza mtoto huyo
Mtoto wa kwanza aliyetengezwa kwa kutumia mbinu ya uzazi wa mbegu za watu watatu amezaliwa ,wanasayasi wamefichua.
Mtoto huyo wa kiume mwenye miezi mitano ana chembe chembe za DNA kutoka kwa mamake,babake pamoja na jeni za mfadhili.
Madaktari wa Marekani walichukua hatua hiyo kuhakikisha kuwa mtoto huyo wa kiume atakuwa huru kutokana na hali ya jeni ambayo mamake kutoka Jordan anabeba katika jeni zake.
Wataalam wanasema kuwa hatua hiyo ni mwamko mpya wa kimatibabu na inaweza kusaidia familia nyengine zilizo na hali za jeni zisizokuwa za kawaida.
Lakini wameonya kuwa uchunguzi wa mara kwa mara wa mbinu hiyo mpya ya kiteknolojia inayoitwa ufadhili wa Mitochondrial unahitajika.
Mitochondria ni vyumba vidogo vidogo ndani ya kila seli ambavyo hubadili chakula kuwa nguvu inayotumika mwilini.
Baadhi ya wanawake hubeba jeni zilizo na kasoro na wanaweza kupitisha jeni hizo hadi kwa watoto wao.

Comments

Popular posts from this blog

NINI MAANA KIGOLI?. AU BINTI KIGOLI

Mambo 10, ya kumfanya mpenzi wako akupende milele@ Kama uliamini mapenzi pesa... SAHAU