Waasi watangaza vita dhidi ya serikali Sudan Kusini
Kundi la waasi nchini Sudan Kusini la Democratic Movement Cobra Faction, limetangaza kuwa litarejelea mapigano dhidi ya serikali ya Rais Salva Kiir.
Kundi hilo linaloongozwa na Luteni Khalid Botrus Bora, limekuwa likipagia haki zaidi za jamii ya Murle, na liliafikiana makubaliano ya amani na serikali ya Juba mwezi Mei mwaka 2014.
Katika taarifa, lilisema kuwa litajiunga na vikosi vingine ambavyo kwa sasa vinapiga na serikali.
Mtandao wa Sudan Tribune unaripoti kuwa tangazo hilo lililotolewa hii leo mjini Nairobi, Kenya, linajiri baada ya aliyekuwa waziri wa kilimo nchini humo Lam Akol, kuunda kundi jipya la waasi baada ya majuma kadha ya mazungumzo na makundi ya upinzani.
Mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yalizuka katika taifa hilo janga zaidi duniani mwezi Disemba mwaka 2013.
Comments
Post a Comment