Lupita Nyong’o amefunguka kwa mara ya kwanza
Lupita Nyong’o amefunguka kwa mara ya kwanza baada ya kutajwa na rapper Jay Z kwenye wimbo wa ‘We Made It’ alioshirikishwa na Jay Electronica.
Akiongea kwenye kipindi cha Jimmy Kimmel Live, muigizaji huyo amesema kuwa hakujua kama rapper huyo amemuimba mpaka pale mdogo wake alipomtumia link ya wimbo huo.
“I felt like the coolest kid ever, I was like, What are you on about? and he sent me the link, and then I heard it!, I’m on my Lupita Nyong’o and I was like, WHAAAAAT?!,” amesema Lupita.
Kwenye wimbo huo Jay Z amerap, “I’m on my Lupita Nyong’o, Stuntin’ on stage got the 12 Years a Slave. This ace of spades look like an Oscar Black tux.”
Comments
Post a Comment