Tamasha la wapenzi wa jinsia moja lavunjwa Uganda

Polisi walivunja tamasha la wanamitindo wa wapenzi ya watu wa jinsia moja na kushika baadhi yao Uganda wiki kadhaa nyumaImage copyrightAP
Polisi nchini Uganda wamevunja tamasha la wapenzi wa jinsia moja.
Watu kadhaa wametimuliwa walipojaribu kuingia katika hoteli moja katika mji wa Entebbe.
Walijaribu kuliandaa tena tamasha hilo katika ufuo wa ziwa Victoria na kwa mara nyengine polisi ikawalazimisha kuondoka.
Maafisa waliyasindikiza mabasi matano yaliojaa watu kuelekea mji mkuu Kampala.
Mapenzi ya watu wa jinsia moja iliharamishwa nchini Uganda chini ya sheria za ukoloni katika kifungu kinachokataza mtu kufanya ngono kinyume na kawaida.
Waziri wa maadili nchini Uganda Simon Lokodo, mwezi uliopita alisema shughuli zote za wapenzi wa jinsia moja ni haramu na kinyume na tamaduni za watu wa Uganda.
Waziri wa maadili nchini Uganda Simon LokodoImage copyrightEMPICS
Image captionWaziri wa maadili nchini Uganda Simon Lokodo
Polisi ilipiga marufuku mkutano wa wapenzi wa jinsi moja katika klabu moja ya usiku mjini Kampala wiki kadhaa zilizopita.
Mwanaharakati wa kupigania haki za wapenzi ya jinsia moja nchini Uganda anasema kuwa watu wenye wapenzi wa jinsia moja wanastahili kuendelea na shughuli zao ikiwa watahitaji kufanya hivyo.
Kupitia mtandao wake wa kijamii Frank Mugisha anasema kuwa ''jamii ya LGBT itaendelea kufanya mikutano yao kama inavyoruhusiwa kikatiba bila pingamizi lolote''
Lakini Waziri wa maadili nchini Uganda amesema kuwa serikali yake haitawafumbia macho wale wanaoshabikia wapenzi wa jinsia moja na kujaribu kusambaza harakati zao alizoita haramu nchini humo.
''Katika jamii yetu maswala ya ngono huwa ni ya siri mno, itakuwaje kuwa sasa maswala ya ngono yanawekewa gwaride ?''
''Tutapambana na mtu yeyote atakayejaribu kuchochea ama hata kufadhili na kupigia debe swala la wapenzi wa jinsia moja''

Comments

Popular posts from this blog

NINI MAANA KIGOLI?. AU BINTI KIGOLI

Mambo 10, ya kumfanya mpenzi wako akupende milele@ Kama uliamini mapenzi pesa... SAHAU