Rais MAGUFULI atumbua wawili kwa kufungua akaunti nyingine ya maafa KAGERA

Rais JOHN MAGUFULI ametengua uteuzi wa Katibu Tawala wa Mkoa wa KAGERA AMANTIUS MSOLE na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya BUKOBA
Rais JOHN MAGUFULI
Rais JOHN MAGUFULI ametengua uteuzi wa Katibu Tawala wa Mkoa wa KAGERA AMANTIUS MSOLE na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya BUKOBA, STEVEN MAKONDA baada ya kubaini kuwa wamefungua akaunti nyingine ya benki kwa kutumia jina linalofanana na akaunti rasmi ya kuchangia maafa iitwayo Kamati Maafa Kagera kwa lengo la kujipatia fedha.
Taarifa iliyotolewa na Waziri Mkuu KASSIM MAJALIWA muda mfupi baada ya kupokea hundi ya msaada kutoka kwa Waziri Mkuu wa INDIA imeeleza kuwa pamoja na kutengua uteuzi huo Rais MAGUFULI ameagiza vyombo vya dola vichukue hatua dhidi ya wote waliohusika katika njama za kufungua akaunti hiyo.

Aidha, Waziri Mkuu MAJALIWA amemsimamisha kazi Mhasibu Mkuu wa Mkoa wa KAGERA, SIMBAUFOO SWAI kutokana na kuhusika katika njama hizo.

Waziri Mkuu ametoa wito kwa wananchi na taasisi mbalimbali kuendelea kuchangia misaada kwa ajili ya walioathirika kwa kutumia akaunti rasmi ya "Kamati Maafa Kagera"ambayo imetangazwa na Serikali.

Comments

Popular posts from this blog

NINI MAANA KIGOLI?. AU BINTI KIGOLI

Mambo 10, ya kumfanya mpenzi wako akupende milele@ Kama uliamini mapenzi pesa... SAHAU