UTAFITI Twaweza: Nchi Haiongozwi Kidikteta Kama Inavyodaiwa

Ripoti ya utafiti mpya wa taasisi ya Twaweza uliozinduliwa leo jijini hapa unaeleza kuwa Watanzania wengi hawaoni kama nchi inaendeshwa kidikteta baada ya mtu mmoja kati ya 10 waliohojiwa kueleza nchi inaongozwa kwa mfumo huo.

Matokeo ya utafiti huo uliofanywa kwa njia ya simu kati ya Septemba 24-29 mwaka yanasema kuwa watu sita kati ya 10 sawa na asilimia 58 walipinga kuwa nchi inaongozwa kidikteta huku asilimia 31 wakieleza kutokuwa na uhakika.

Katika utafiti huo unaoitwa "Demokrasia, udikteta na maandamano: wananchi wanasemaje", mwananchi mmoja kati ya watatu alitafsiri udikteta kuwa ni kitendo cha Serikali kutumia nguvu  wakati wa kuitawala nchi.

Licha ya wananchi wengi kueleza hawaoni nchi ikiongozwa kidikteta, ripoti hiyo iliyohoji watu 1,602 wa Tanzania Bara inaeleza kuwa wananchi saba kati ya 10 wanaunga mkono demokrasia kama mfumo bora wa Serikali, mtazamo ambao unaoshabihiana na wafuasi wa vyama mbalimbali nchini.

Sanjari na kuhoji masuala mbalimbali namna ya uendeshwaji wa nchi, Twaweza walihoji watu pia ufuasi wao kwa vyama vya siasa ambapo asilimia 66 walieleza kuwa karibu na CCM huku asilimia 19 wakiwa karibu na upinzani hususan Chadema. Watu wawili kati ya 10 (asilimia 15) walisema hawana ukaribu na chama chochote.   

Comments

Popular posts from this blog

NINI MAANA KIGOLI?. AU BINTI KIGOLI

Mambo 10, ya kumfanya mpenzi wako akupende milele@ Kama uliamini mapenzi pesa... SAHAU