TANESCO yaagizwa kuwafuata wananchi vijijini na kuwaunganishia umeme
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. MEDARD KALEMANI amewaagiza wafanyakazi wa shirika la umeme nchini TANESCO
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. MEDARD KALEMANI
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. MEDARD KALEMANI amewaagiza wafanyakazi wa shirika la umeme nchini TANESCO kuanza utaratibu wa kuwafuata wananchi vijijini na kuwaunganishia umeme badala ya kukaa maofisini na kusubiria wananchi wawafuate.
Dkt. KALEMANI ametoa agizo hilo wakati akizungumza na wakazi wa vijiji vya LOSINYAI na KILOMBERO wilaya ya SIMANJIRO mkoani MANYARA ambapo amesema umeme ni nyenzo na nishati muhimu ya kuharakisha maendeleo ya kuipeleka nchi kuwa na uchumi wa wa kati ifikapo mwaka 2025.
Mbunge wa SIMANJIRO mkoani MANYARA,JAMES MILYA,ameishukuru serikali ya awamu ya TANO kwakupeleka mradi wa umeme vijijini REA ambapo amesema utawasaidi watoto kusoma hasa nyakati za usiku huku Mkuu wa wilaya ya SIMANJIRO,ZEPHANIA CHAULA akiwaasa wananchi kuitunza miundombinu hiyo na atakayebainika kuiharibu atachukuliwa hatua.
Vijiji 21 vilivyopo katika wilaya ya SIMANJIRO mkoani MANYARA vimepatiwa umeme na vijiji 32 vinavyobaki vitapata umeme wa REA ktika awamu ya TATU.

Comments
Post a Comment