Viongozi mashuhuri wafika mazishi ya Shimon Peres
Viongozi mbalimbali duniani wanajiandaa kutoa heshima zao za mwisho wakati wa mazishi ya kiongozi shupavu wa Israeli marehemu, Shimon Peres, aliyefariki Jumatano wiki hii.
Kuna ulinzi mkali katika eneo ambalo litatumika kwa mazishi yake, katika maeneo ya makaburi ya kitaifa mlimani Herzl mjini Jerusalem.
Waombolezaji watajumuisha Rais wa sasa wa Marekani Barack Obama na Rais wa zamani Bill Clinton, aliyefanya kazi na Bw Peres katika mkutano wa mwafaka wa amani wa Oslo mwaka wa 1993.
Viongozi kadhaa wa Kipalestina pia watahudhuria mazishi hayo akiwepo Rais Mahmoud Abbas na mpatanishi mkuu wa zamani Saeb Erekat.
Itakuwa mara ya kwanza kwa Bw Abbas kuzuru Israel tangu 2010.
Maelfu ya Waisraeli walitoa heshima zao za mwisho kwa hayati Peres, ambaye maiti yake imekuwa nje ya majengo ya Bunge la Israeli, Knesset.
Polisi wa Israel wamesema maafisa 8,000 wanatumiwa kudumisha usalama.
Mazishi hayo ndiyo makubwa zaidi kuwahi kufanyika Israel tangu mazishi ya waziri mkuu Yitzhak Rabin, aliyeuawa na Myahudi 1995.
Bw Peres alifariki Jumatano baada ya kuugua kiharusi kwa muda wa wiki mbili.
Wageni mashuhuri:
- Barack Obama, Rais, Marekani
- Bill Clinton, rais wa zamani, Marekani
- Mwanamfalme Charles, Uingereza
- Boris Johnson, Waziri wa mambo ya nje, Uingereza
- Tony Blair, waziri mkuu wa zamani, Uingereza.
- Malcolm Turnbull, Waziri Mkuu, Australia
- Justin Trudeau, Waziri Mkuu, Canada
- Donald Tusk, Rais, Baraza la Umoja wa Ulaya
- Francois Holland, Rais, Ufaransa
- Joachim Gauck, Rais, Ujerumani
- Matteo Renzi, Waziri Mkuu, Italia
- Jenerali Nakatani, waziri wa zamani wa ulinzi, Japan
- Jawad Anani, waziri wa ngazi ya juu, Jordan
- Enrique Pena Nieto, Rais, Mexico
- Jens Stoltenberg, Katibu Mkuu, Nato
- Mark Rutte, Waziri Mkuu, Uholanzi
- Valentina Matviyenko, spika, bunge la juu, Urusi
- Mfalme Felipe VI, Uhispania
- Ban Ki-moon, Katibu Mkuu, Umoja wa Mataifa
Who was Shimon Peres?
- Born in 1923 in Wisniew, Poland, now Vishnyeva, Belarus
- First elected to the Knesset (Israeli parliament) in 1959
- Served in 12 governments, including once as president and twice as prime minister
- Seen as a hawk in his early years, when he negotiated arms deals for the fledgling nation
- In 1996 he ordered the so-called Operation Grapes of Wrath operation against Beirut in retaliation for Lebanese Hezbollah's escalated rocket fire on northern Israel. The bombing campaign killed and injured hundreds of civilians
- A member of the government that approved the building of Jewish settlements on occupied territory, but came to view their future as negotiable
- Played a key part in reaching the Oslo peace accords, the first deal between Israel and the Palestinians, which said they would "strive to live in peaceful coexistence"
Comments
Post a Comment