Mwamko wa wasichana katika teknolojia Tanzania
Mwamko wa wasichana katika teknolojia Tanzania
- 30 Septemba 2016
Azma yao ni kufundisha wasichana wengi iwezekanavyo maswala ya teknolojia.
Kuandika programu za kompyuta na simu, kutengeneza programu tumishi na hata kubuni na kutengeneza mitandao.
Wakiwa wameanza miaka mitatu tu iliyopita, Apps & Girls ni shirika lisilo la kiserikali ambalo tayari limewafikia wasichana zaidi ya 600 kupitia mtandao wa shule za sekondari takribani 17.
Mwanzilishi wa Apps & Girls Carolyne Ekyarisiima amezungumza na BBC kuelezea wanafanyaje kuongeza mwamko wa wasichana katika teknolojia nchini Tanzania.
Comments
Post a Comment