Filamu za Bollywood zinazowashirikisha waigizaji maarufu kama Deepika Padukone, kulia, ni maarufu sana Pakistan

Mzozo Kashmir: Pakistan yapiga marufuku filamu za India

Image copyrightAP
Image captionFilamu za Bollywood zinazowashirikisha waigizaji maarufu kama Deepika Padukone, kulia, ni maarufu sana Pakistan
Majumba makuu ya cinema nchini Pakistan yamepiga marufuku filamu za India, kama ishara ya kuonyesha umoja wao na vikosi vya Pakistan katika mzozo unaoshuhudiwa katika eneo la Kashmir.
Marufuku hiyo imetangazwa katika miji ya Lahore, Karachi na Islamabad.
Hatua hiyo inafuatia mzozo unaozidi kutotkota kati ya India na Pakistan.
Siku ya Ijumaa, watayarishaji wa filamu kutoka India walipiga marufuku waigizaji wa Pakistan kufanya kazi Bollywood.
Mwanasiasa mmoja wa mrengo wa kulia, amewaamrisha waigizaji wa Pakistan kuondoka India.
Mhariri wa BBC kusini mwa bara Asia Charles Haviland anasema kwamba sio mara ya kwanza ambapo mzozo kati ya India na Pakistan umeathiri utamaduni wa mataifa hayo mawili.
Mwandishi wa BBC anasema filamu za India ni maarufu sana Pakistan, kwani sekta ya filamu nchini Pakistan haijaimarika kiasi cha kutoa ushindani kwa Bollywood.
Hata hivyo wasimamizi wa maeneo ya Cinema nchini Pakistan wamekiri kwamba huenda wakapata hasara kubwa kutokana na umaarufu wa filamu za India.
Eneo la Kashmir limekuwa kitovu cha vita baina ya mataifa hayo mawili, na tiyari limesababisha vita mara mbili.
Mapema ijumaa, wanakijiji wa India wanaoishi kwenye mpaka wa mataifa hayo mawili walikimbia baada ya ripoti kwamba India imeanzisha mashambulizi dhidi ya wapiganaji katika eneo la Kashmir.
Raia wa India waabiri gari lililotolewa na serikali yao karibu na mpaka na Pakistan.Image copyrightEPA
Image captionRaia wa India wanaoishi karibu na mpaka wa Pakistan waondolewa wakati hali ya wasiwasi inashuhudiwa kati ya pakistana na India kutokana na mzozo wa eneo la Kashmir.

Comments

Popular posts from this blog

NINI MAANA KIGOLI?. AU BINTI KIGOLI

Mambo 10, ya kumfanya mpenzi wako akupende milele@ Kama uliamini mapenzi pesa... SAHAU