Watumishi wa umma wachangisha zaidi ya Bil 1 kusaidia waathirika wa tetemeko


Katibu Mkuu Kiongozi Balozi JOHN KIJAZI amewasilisha kwa Waziri Mkuu hundi ya zaidi ya shilingi bilioni moja ikiwa ni michango ya watumishi wa umma
Waziri Mkuu KASSIM MAJALIWA, akikabidhiwa mfano wa hundi na Katibu Mkuu Kiongozi aliyeongozana na Msajili wa Hazina LAWRENCE MAFURU
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi JOHN KIJAZI amewasilisha kwa Waziri Mkuu hundi ya zaidi ya shilingi bilioni moja ikiwa ni michango ya watumishi wa umma kutoka katika wizara, idara na taasisi zote za umma nchini kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi la Septemba 10 mkoani KAGERA.

Akikabidhi hundi hiyo kwa Waziri Mkuu KASSIM MAJALIWA, Katibu Mkuu Kiongozi aliyeongozana na Msajili wa Hazina LAWRENCE MAFURU amesema wafanyakazi wameguswa na janga hilo na hivyo kuwasaidia wananchi hao ili kukabaliana na changamoto iliyowapata.
Katibu Mkuu Kiongozi amesema michango mingine inaendelea kuchangwa ambapo ikikamilika itakabidhiwa kwa Waziri Mkuu kwa malengo ya kusaidia waliokumbwa na janga hilo.

Kwa upande wake Waziri Mkuu MAJALIWA amesema ni jambo la faraja kwa wafanyakazi wa umma kuamua kujitolea kwa ajili ya wengine ambapo amemhakikishia Balozi KIJAZI kuwa michango hiyo itafikishwa kwa walengwa katika utaratibu uliopangwa

Comments

Popular posts from this blog

NINI MAANA KIGOLI?. AU BINTI KIGOLI

Mambo 10, ya kumfanya mpenzi wako akupende milele@ Kama uliamini mapenzi pesa... SAHAU