Simba yaishtukia Yanga mapema, yamficha Ajib

NA HUSSEIN OMAR
SIMBA imeshtuka mapema kabisa naimeamua kumficha straika wake tegemeo, Ibrahim Ajib, ili kumwepusha na kadi nyingine ya njano ambayo inaweza kumsababisha akakosa pambano la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Yanga litakalochezwa Oktoba 1, mwaka huu katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Ishu kamili iko hivi:-Ajib ana kadi mbili za njano iwapo akipata kadi nyingine ya tatu kwenye mchezo unaofuata dhidi ya Majimaji,basi atalazimika kukaa nje kwenye pambano la Oktoba 1, dhidi ya Yanga kutokana na adhabu ya kufungiwa mechi moja ambayo itaambatana na kadi hiyo.
Katika kuhakikisha hilo halitokei, inaonekana Simba wameamua kumweka benchi kwenye mechi dhidi ya Majimaji ili asiwe hatarini kulikosa pambano la kisasi dhidi ya Yanga mwanzoni mwa mwezi ujao.
Hilo limethibitika kwenye mazoezi ya timu hiyo jana jioni katika Uwanja wa Boko Veteran nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, baada ya kocha wa Simba, Joseph Omog, kuonekana kumwandaa Ame Ali kuziba nafasi ya Ajib katika mchezo ujao dhidi ya Majimaji.
Omog alitumia mazoezi hayo kuandaa kombinesheni kali katika safu yake ya ushambuliaji ambayo inawahusisha Ame Ali naMrundi, Laudit Mavugo ambao wanatarajiwa kuongoza jahazi la Simba kwenye mchezo wao unaofuata wa VPL.
Katika mazoezi hayo, Mavugo alionekana kuwa moto wa kuotea mbali kutokana na staili mbalimbali za kufunga alizokuwa akizitumia, huku Ajib ambaye licha ya kuonekana kuwa hatacheza dhidi ya Majimaji, naye hakubaki nyuma kwenye mazoezi hayo na kuendeleza moto wake ambao unawanyima usingizi Yanga.
Mbali na Ajib kwenye mazoezi hayo, Omog pia alionekana kujiandaa kumpumzisha Shiza Kichuya kwenye mchezo dhidi ya Majimaji kutokana na kumtumia zaidi Hijja Ugando kwenye winga ya kushoto, huku Hamad Juma akicheza kama beki wa kulia.
Kanuni za ligi kuu zinamzuia mchezaji kucheza mechi moja iwapo atapata kadi tatu za njano kwenye ligi na mchezaji atakosa mechi hadi tatu ikiwa atapata kadi nyekundu ya moja kwa moja katika mechi.
Kutokana na hali hiyo, ndiyo maana kadi mbili za njano za Ajib zimekuwa zikiwapa presha Simba kwa sababu kama akipata nyingine anaweza kukosa mchezo dhidi ya Yanga utakaopigwa Oktoba 1, mwaka huu.

Comments

Popular posts from this blog

NINI MAANA KIGOLI?. AU BINTI KIGOLI

Mambo 10, ya kumfanya mpenzi wako akupende milele@ Kama uliamini mapenzi pesa... SAHAU