Rais MAGUFULI amtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa NJOMBE


Rais Dkt. JOHN MAGUFULI ametumia salamu za rambirambi kwa familia zilizopatwa na msiba kufuatia ajali ya basi la Kampuni ya New Force
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. JOHN POMBE MAGUFULI
 Rais Dkt. JOHN MAGUFULI ametumia salamu za rambirambi kwa familia zilizopatwa na msiba kufuatia ajali ya basi la Kampuni ya New Force iliyotokea usiku wa kuamkia leo katika Kijiji cha LILOMBWI, Kata ya KIFANYA, tarafa ya IGOMINYI Mkoani NJOMBE.
       
Basi hilo lililokuwa linatokea jijini DSM kwenda SONGEA  mkoani RUVUMA lilipinduka na kuuwa watu 12 na wengine 28 kujeruhiwa.

Taarifa iliyotolewa na Ikulu imesema  katika salamu hizo kupitia kwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dkt. REHEMA NCHIMBI, Rais MAGUFULI amesema amepokea taarifa za ajali hiyo kwa masikitiko na kwamba anaungana na familia, ndugu, jamaa na marafiki wote waliopatwa na msiba katika kipindi kigumu cha majonzi.
         
Aidha Rais Magufuli  amewapa pole majeruhi wote na amewaombea wapone haraka ili waweze kuungana na familia zao na kuendelea na shughuli zao za kila siku

Comments

Popular posts from this blog

NINI MAANA KIGOLI?. AU BINTI KIGOLI

Mambo 10, ya kumfanya mpenzi wako akupende milele@ Kama uliamini mapenzi pesa... SAHAU