Serikali yawaondolea vikwazo wawekezaji

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Dkt. JULIANA PALLANGYO amesema serikali imeondoa vikwazo kwa wawekezaji nchini
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Dkt. JULIANA PALLANGYO
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Dkt. JULIANA PALLANGYO amesema serikali imeondoa vikwazo kwa wawekezaji nchini na kuweka mazingira rafiki ya kufanya biashara ili kuleta maendeleo katika sekta mbalimbali nchini.

Akizungumza mara baada ya kufungua semina ya makubaliano ya Biashara ya Nishati kati ya TANZANIA na NORWAY Dkt PALLANGYO amesema serikali imeunda sera za kitaifa na sheria mbalimbali ili kuwawezesha wawekezaji hao kufanya biashara kwa kufuata sheria za nchi.

Naye Katibu Mkuu wa wizara ya Viwanda na Biashara Prof. JOSEPH MKENDA amesema mkutano huo utajadili namna wawekezaji kutoka NORWAY wanaweza kuwekeza nchini TANZANIA husuani katika sekta ya nishati.

Comments

Popular posts from this blog

NINI MAANA KIGOLI?. AU BINTI KIGOLI

Mambo 10, ya kumfanya mpenzi wako akupende milele@ Kama uliamini mapenzi pesa... SAHAU