Diana ndiye Miss Tanzania 2016

ALIYEKUWA Miss Kinondoni, Diana Edward ndiye mlimbwende wa Tanzania 2016 baada ya kuwashinda wenzake 29 katika viwanja vya Rock City Mall juzi usiku mkoani hapa.

Mashindano hayo makubwa kabisa hapa nchini yaliamuliwa na majaji ambao ni Rita Mbelo,Catherine Kibaso,Sophia Masei,Raphael Siantini,Joe Makanyaga,Eliza Kilili,Juma Sultan,Prashant Patel na Ramesh Shah.
Mashindano hayo yalianza kwa warembo kucheza nyimbo mbali mbali kabla ya kutinga na mavazi ya ubunifu,ufukweni na vazi la jioni. Jaji Shah aliweza kuwataja warembo walioingia 15 bora ambao ni Anna Nitwa,Sia Pius,Lisa Ndolo,Grace Malikita,Eunice Robert,Regina Ndimbo,Iluminata Dominic,Sporah Lulende na Maria Peter.
Wengine ni Maureen Ayoub,Queen Nazir,Julietha Kabete,Maureen Kamanya na Abel John. Patel aliwataja warembo walioingia 5 bora ambao ni Grace Malikita,Anna Nitwa,Maria Peter,Julietha Kabete na Diana Edward.
Jaji Prashant Patel aliweza kutangaza warembo walioingia tatu bora, ambao ni Diana Edward aliyeibuka mshindi, huku nafasi ya pili ikachukuliwa na Grace Malikita wakati Maria Peter alimaliza watatu.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,Annastazia Wambura aliomba mshindi wa shindano hilo ajitahidi kuzingatia nidhamu na uzalendo hasa pale atakapo wakilisha nchini katika mashindano ya mrembo wa dunia.
Wambura alisisitiza waandaaji wa mashindano hayo waendelee kufuata taratibu za mashindano na kuhakikisha wanatekeleza mikataba waliosaini na warembo hao.
Wambura ameomba mashindano hayo yafanyike katika mikoa mengine pia tofauti na hapa. Diana alikabidhiwa gari aina ya Toyota IST yenye thamani ya Sh milioni 14

Comments

Popular posts from this blog

NINI MAANA KIGOLI?. AU BINTI KIGOLI

Mambo 10, ya kumfanya mpenzi wako akupende milele@ Kama uliamini mapenzi pesa... SAHAU