Mike Pence: Democratic iliteua mgombea mwenye mashaka

Uchaguzi ni Novemba 8, 2016
Image captionUchaguzi ni Novemba 8, 2016
Huku zikiwa zimesalia siku chache kuelekea uchaguzi mkuu wa Marekani wakati mgombea wa chama Democratic Bi Hillary Clinton na Donald Trump wa Republican wakiendelea na kampeni zao,mgombea mwenza wa Trump, Mike Pence amesema kuwa tangazo la shirika la kijasusi la Marekani FBI kuhusiana na kashfa mpya za barua pepe zinazomhusisha Bi Clinton, ni wazi kwamba chama hicho kiliteua mgombea mwenye mashaka.
Hata hivyo pamoja na shutuma hizo dhidi ya Bi Clinton, lakini meneja kampeni wake John Podesta, ameliambia shirika la habari la CNN kwamba mkurugenzi mkuu wa FBI James Comey, anapaswa kutoa ufafanuzi kuhusiana na hatua yake ya kutoa tangazo tata siku chache kuelekea uchaguzi.
Kwa upande wake Mike Pence amesisitiza kuwa sakata la email dhidi ya Bi.Clinton tangu mwanzo imekuwa ni faida katika kampeni zao na zimewasogeza mbele.
Naye mgombea mwenza wa Bi.Clinton pia Tim Kaine,amebeza tangazo hilo la FBI linaloibua kashafa mpya ya barua pepe dhidi ya Hillary, lililotolewa siku chache kuelekea uchaguzi mkuu na kusema halina maana yoyote.
Tangu kuanza kwa kampeni za uchaguzi mkuu nchini Marekani, kumekuwa na tambo nyingi kati ya wagombea hawa wawili ambapo, uamuzi kamili ni katika sanduku la kura hapo Novemba 8.mwaka huu.

Comments

Popular posts from this blog

NINI MAANA KIGOLI?. AU BINTI KIGOLI

Mambo 10, ya kumfanya mpenzi wako akupende milele@ Kama uliamini mapenzi pesa... SAHAU