Yanga yaichana Mbao

MABINGWA wa soka Tanzania Bara, Yanga jana waliendelea kuchanja mbuga katika Ligi Kuu baada ya kuichana Mbao FC kwa mabao 3-0 katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Tofauti kabisa na Simba,ambayo ilipata shida sana kuifunga Mbao kwenye uwanja huo hadi kusubiri dakika za lala salama kupata bao la ushindi, Yanga wamepata mabao matatu licha ya kutiliwa ngumu katika kipindi cha kwanza.
Kwa ushindi huo, Yanga sasa imefikisha jumla ya pointi 27 na kubakiza pointi tano tu kabla ya kuikamata Simba inayoongoza msimamo wa ligi hiyo.
Yanga katika mchezo huo wa jana waliandika bao la kwanza kupitia kwa Vicent Bossou aliyefunga kwa kichwa baada ya mpira wa adhabu uliopigwa na Haruna Niyonzima.
Mbuyu Twite aliifungia Yanga bao la pili katika dakika ya 55 baada ya kurusha mpira huo mithili ya kona na kumgonga kipa wa Mbao, Emmanuel Mseja na kujaa wavuni. Dakika 75, Amiss Tambwe aliifungia Yanga bao la tatu na kuzidi kuiweka Yanga katika nafasi nzuri ya kuondoka na pointi tatu.
Bao hilo lilitokana na kazi nzuri ya Niyonzima katikati ya uwanja na kutoa pasi kwa mfungaji. Dakika ya 79, Mbao nusura wapate bao la kufutia machozi baada ya Ndikumana kupiga mpira wa adhabu lakini ukadakwa na kipa Dida.
Yanga: Deogratius Munishi 'Dida', Hassan Kessy/Thaban Kamusoko, Mwinyi Hajji Mngwali, Andrew Vincent, Vincent Bossou, Mbuyu Twite, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Amisi Tambwe, Obrey Chirwa na Deus Kaseke/Mahadhi.
Mbao: Emmanuel Mseja, Steve Mganya, Steve Kigocha, Asante Kwasi, David Majige, Yossouf Ndikumana, Dickson Ambundo, Salmin Hoza, Venance Ludovic/ Frank Damas na Pius Buswita

Comments

Popular posts from this blog

NINI MAANA KIGOLI?. AU BINTI KIGOLI

Mambo 10, ya kumfanya mpenzi wako akupende milele@ Kama uliamini mapenzi pesa... SAHAU