RC Arusha Mrisho Mashaka Gambo, asiimamisha kazi watumishi watatu wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo akitangaza kuwasimamisha kazi watumishi watatu wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro kwa tuhuma za ubadhilifu wa fedha za uchaguzi wa mwaka 2015.
Watumishi hao ni pamoja na Bi. Hadija Mkumbwa ambae alikuwa msimamizi wa uchaguzi wa mwaka 2015 na kumfuta cheo hicho,bwana Evansi Mwalukasa alikuwa mwekahazina wa halmashauri na bwana Sembeli Sinayo yeye alikuwa mwanasheria wa halmashauri.
Maamuzi hayo yamefikia baada yakubainika kuna upotevu wa fedha za uchaguzi takribani Milioni 188 ambazo matumizi yake hayakuwekwa wazi na pia Milioni 20 zilitumika kwa manunuzi ambayo hayakufuata taratibu za manunuzi ya serikali.
“Kuanzi sasa nawasimamisha kazi hawa watumishi watatu kwasababu wameisababishia serikali hasara ya takribani Milioni 128 ambazo zilikuwa fedha za uchaguzi”.
Aidha Mhe. Gambo alisema maamuzi hayo yametokana na taarifa aliyokabidhiwa na kamati aliyoiunda ya kuchunguza mapato na matumizi ya fedha za halmashauri hiyo na kubaini upotevu huo wa fedha nyingi ambazo amesema zingeweza kusaidia shughuli mbalimbali za uchaguzi katika Wilaya hiyo.
Amsema fedha nyingine zimetumika kwenye manunuzi ambayo hayakufuata taratibu na sheria za manunuzi ya serikali kinyume kabisa na taratibu za serikali katika maswala ya manunuzi.
Mhe. Gambo pia kasisitiza watumishi wa serikali kufuata taratibu, sheria na kanuni mbalimbali katika kutekeleza majukumu yao ili kuepuka migongano na uvunjifu wa sheria mahala pa kazi na kupelekea kupoteza ajira zao
Comments
Post a Comment