Picha za wanyama za kuchekesha zaidi 2016
Huu hapa ni mkusanyiko wa picha za kuchekesha na kusisimua za wanyama zilizopigwa mwaka huu, miongoni mwa picha hizi ikiwa moja ya mbweha aliyeingia kichwa kwanza kwenye theluji na nyingine ya nyati aliyegeuzwa choo na ndege mmoja.
Picha hizi zimeteuliwa kushindania tuzo ya picha za ucheshi za wanyama mwaka huu.
Shindano hili huandaliwa kuchangisha pesa na kusaidia shirika la kutetea uhifadhi wa wanyama la Wakfu wa Born Free.
Kuna jumla ya picha 40 na mshindi atatangazwa mwez Novemba.
Hapa ni baadhi ya picha hizo.
Unapokuwa na siku mbaya...ndege anakugeuza choo.
Siku inayofuata baada yako kulewa usiku kucha, na uliambia watu hutakunywa pombe tena...
Umewahi kukutana na sungura mwenye madoido?
Unapojifanya huna kichwa na huoni yanayoendelea ... kama penguini hawa?
Kupata lifti halisi...
Unapojaribu kumuonesha mwenzako kucha zako zilivyopambwa, mwenzako hana haja...
Siku ambayo mambo hayaendi sawa, dubu huyu anashindwa kumnasa samaki...
Unapojificha na kuvunja ahadi yako ya kutokula sana ili usiongeze uzani
Mamako akitaka usione kitu cha kuogofya au cha 'watu wazima' kwenye TV
Comments
Post a Comment