Mdee Kusota Lupango mpaka Juma Tatu



Mbunge wa Jimbo la Kawe Jijini Dar es Salaam Halima Mdee alikamatwa na jeshi la polisi hivi karibuni, kwa kile kinachodaiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Hapi kuwa alitoa maneo ya uchochezi yenye kumtusi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli katika hotuba yake aliyoitoa kwa waandishi wa Habari Julai 4.

Ambapo Mkuu wa Wilaya kwa mujibu wa sheria aliagiza Mbunge huyo ashikiliwe na ahojiwe kwa masaa 48 yaliyotajwa kisheria na kumpa mamlaka Mkuu wa Wilaya kufanya hivyo.


Siku ambayo Mbunge huyo inabidi aachiwe na Jeshi la Polisi imeangukia kwenye sikukuu ya Saba Saba, jambo ambalo linapelekea Mbunge huyo kuendelea kusota rumande mpaka siku ya Jumatatu.

Comments

Popular posts from this blog

NINI MAANA KIGOLI?. AU BINTI KIGOLI

Mambo 10, ya kumfanya mpenzi wako akupende milele@ Kama uliamini mapenzi pesa... SAHAU