al Hussein:chuki za makabila ni hatari Sudan Kusini

Salva KiirImage copyrightGOOGLE
Image captionRais wa Sudan Kusini Salva Kiir
Kamishina wa juu wa haki za binadamu wa umoja wa mataifa Prince Zeid Ra'ad al Hussein ameonya kuwa kuzuka kwa kauli za chuki na uchochezi wa ghasia za kikabila nchini Sudan kunaweza kusababisha mauaji ya halaiki.
Hofu baina ya makabila makubwa Dinka, na yale ya kutoka ukanda wa ikweta imeongezeka kwa kasi katika wiki za hivi karibuni, baada ya shambulio la basi huko Dinka na kusababisha vifo vya watu kadhaa waliokuwa wakisafiri.
Umoja wa mataifa unasema kuwa una wasiwasi juu ya mashambulio hayo na kuhusu barua za kuogofya watu kutoka ukanda wa Ikweta inaonekana kuwa ni kulipiza kisasi.
Pia amesema kuwa ametilia maanani kauli iliyotolewa na Rais wa nchi hiyo Salva Kiir ambayo imetafsiriwa na wengi kama ina msukumo wa kikabila. Rais Kiir alisema yeye mwenyewe ataendesha operasheni ya kijeshi dhidi ya makundi ya waasi kuwajibika kwa mauaji katika eneo hilo

Comments

Popular posts from this blog

NINI MAANA KIGOLI?. AU BINTI KIGOLI

Mambo 10, ya kumfanya mpenzi wako akupende milele@ Kama uliamini mapenzi pesa... SAHAU