Mimi ni Mwanamke Nisiyeweza Ficha Hisia zangu Hata Mkiniona Mshamba – Shamsa Ford

Msanii wa filamu na mama wa mtoto mmoja Shamsa Ford amesema yeye ni mwanamke ambaye hawazi kufisha hisia zake za mapenzi.


Malkia huyo wa filamu ambaye alifunga ndoa miezi mitatu iliyopita na mfanyabishara wa maduka ya nguo Chidi Mapenzi, amesema amekuwa akijiachia katika mitandao ya kijamii kueleza hisia zake juu mume wake kutokana na kudai kushindwa kuzizuia hisia zake.

“Kuna muda huwa natamani dunia nzima ijue ni jinsi gani nakupenda na kukuthamini kwasababu mimi ni mwanamke nisiyeweza ficha hisia zangu hata mkiniona mshamba,” aliandika Shamsa kupitia instagram.

Aliongeza, “Ulikutana na wasichana wengi katika maisha yako lakini ni mimi pekee ndo niliyepata bahati ya kuwa mke wako. Naomba niseme naheshimu siku uliyonitamkia unanipenda, naheshimu siku uliyonitolea barua, naheshimu siku uliyonitolea mahali lakini kubwa kuliko vyote naheshimu siku uliyoapa ndani ya nyumba ya Mungu (Msikiti) kuwa mimi ndo mke wako. Hakika Mungu ndiye aliyetuonganisha mimi na wewe na inshaallah kwa kudra zake tutazikana, nakupenda mume wangu kipenzi aliyenipa Mungu,”

Pia mwigizaji huyo amewataka mashabiki wake wa filamu kukaa makao wa kula kwa ajili ya ujio ya filamu zake mpya

Comments

Popular posts from this blog

NINI MAANA KIGOLI?. AU BINTI KIGOLI

Mambo 10, ya kumfanya mpenzi wako akupende milele@ Kama uliamini mapenzi pesa... SAHAU