Jah Prayzah amshukuru Diamond kwa kumweka kwenye ramani ya Afrika

Ukishikwa mkono na waliokutangulia na wewe shika wengine walio nyuma yako
Davido kupitia Number One Remix, alimtambulisha Diamond kwenye ramani ya Afrika. Baada ya miaka michache, Diamond pia amefanikiwa kuwatambulisha zaidi wasanii wengine kwenye jicho pana la muziki wa bara hilo.
Miongoni mwao ni Akothee wa Kenya na Jah Prayzah wa Zimbabwe.
Jina la Prayzah limekuwa kubwa nje ya Zimbabwe mwaka huu baada ya kumshirikisha Diamond kwenye wimbo wake Watora Mari. Kama hiyo haitoshi, muimbaji huyo hivi karibuni alishinda tuzo ya MTV MAMA (Listener’s Choice) – na anadhani haijaja kwa bahati mbaya bali Diamond amechangia.
Amemweleza Diamond kama ni mtu wa pekee.
“Big shout out to @diamondplatnumz,” ameandika kwenye Twitter. “It’s no coincidence that in the same year Watora Mari made waves, I got the MAMA award. You are amazing

Comments

Popular posts from this blog

NINI MAANA KIGOLI?. AU BINTI KIGOLI

Mambo 10, ya kumfanya mpenzi wako akupende milele@ Kama uliamini mapenzi pesa... SAHAU