Simu za Samsung Galaxy Note 7 ni marufuku Tanzania
Image copyright GETTY IMAGES Image caption Samsung imesema haitaunda tena simu aina ya Galaxy Note 7 Tanzania na Rwanda zimepiga marufuku uingizaji, usambazaji na utumiaji wa simu za Samsung aina ya Galaxy Note 7. Hatua hiyo imechukuliwa baada ya visa vya simu hizo kulipuka na kushika moto kuripotiwa nchi mbalimbali, jambo lililoifanya kampuni hiyo kutangaza haitaunda tena simu hizo. Aidha, Samsung iliwashauri wote waliokuwa wamenunua simu hizo kuzizima na kutozitumia tena. Nchi hizo mbili za Afrika Mashariki zimefikia uamuzi huo katikati ya wiki iliyopita huku nchi nyingine kama Kenya zikisema hatua ambazo kampuni ya Samsung imezichukua hadi sasa zinatosha. Samsung: Zimeni simu za Note 7 ni hatari Rwanda yapiga marufuku Galaxy Note 7 Kwa mujibu wa gazeti la The East African, Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano TanzaniaBw Innocent Mungy, amewataka wananchi wote ambao wamenunua simu hizo kuzizima na kuzirudisha katika maduka waliyonunulia na wauzaji hao kufuat...