AMEKUBALI…….Messi kurudi kikosi cha Argentina

BUENO AIRES, Argentina
BAADA ya kuwapo maandamano ya mamia ya mashabiki nchini Argentina  na wito mbalimbali kutoka kwa wadau wa soka akiwamo Rais wao Mauricio Macri, kumshinikiza straika wao, Lionel Messi, arejee kwenye kikosi cha timu ya taifa, taarifa zinasema kuwa staa huyo hatimaye amekubali kubadili uamuzi wake.
Hata hivyo, kwa mujibu wa taarifa hizo zilizochapishwa na gazeti la kila siku nchini humo, La Nacion, Messi  atazikosa mechi za kufuzu  fainali za Kombe la Dunia zitakazopigwa Septemba, 2018, lakini atakuwa amejiunga na kikosi hicho kuanzia Novemba mwaka huu.
Taarifa katika gazeti hilo zilikwenda mbali zaidi zikieleza jinsi  Messi ambavyo anaziwazia fainali hizo za Kombe la Dunia za mwaka  2018 zitakazofanyika nchini  Urusi na huku gazeti hilo la  La Nacion, likidai kuwa habari hizo lilizipata kutoka kwa mchezaji aliyepo karibu na staa huyo na ambaye wamecheza naye fainali za Kombe la Dunia mara tatu.
“Ni kweli Messi ameshabadili uamuzi na amekubali kuichezea tena Argentina ila atazikosa mechi za kufuzu fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika Septemba, 2018,” kilieleza chanzo hicho kwa mujibu wa gazeti hilo.
Messi aliamua kukitema kikosi cha Argentina  mwezi uliopita baada ya kupokea kipigo kutoka kwa mahasimu wao, Chile  katika mechi ya fainali ya michuano ya Kombe la  Copa America.
Hatua hiyo iliwafanya watu wenye majina akiwamo rais wake na wachezaji nyota wa zamani, Ronaldo na Diego Maradona kuelezea ndoto zao za kushuhudia Messi akirejea katika uzi wa  Argentina.

Comments

Popular posts from this blog

NINI MAANA KIGOLI?. AU BINTI KIGOLI

Mambo 10, ya kumfanya mpenzi wako akupende milele@ Kama uliamini mapenzi pesa... SAHAU