CIA Walimuua Mwanamuziki Bob Marley?

Kwa muda wa miaka kama 20 hivi nimekua mshabiki na mfuatiliaji sana wa muziki wa reggae na waimbaji wake. Nimesoma taarifa mbalimbali juu ya waimbaji wa muziki huu hasa Robert Nesta Marley (Bob Marley) lakini leo nimekutana na taarifa iliyo nishtua kidogo juu ya kifo cha muasisi huyo.

Sote tunajua kwamba bob alifariki kwa kansa iliyo sababishwa na uvutaji wake wa bangi uliopindukia , lakini kwa mujibu wa jarida la high times, bangi haikusababisha kansa iliyomuua bob.

Jarida la ripoti kwamba kansa hiyo ilipandikizwa na aliejifanya muandishi wa habari kwa kumpelekea zawadi ya viatu vilivyo kuwa na waya ndani uliowekewa vimelea vya cancer, waya huo mlimchoma bob kidoleni alipokua akijaribisha zawadi hiyo aliyopewa, baadae mwandishi huyo alipochunguzwa aligundulika ana uhusiano na CIA waliofanya jaribio la kumuua bob (ambush in the night)

Bob kwa kujua alisha nasa kwenye mtego wa maadui wake waliokua wanamuwinda usiku na mchana aliamua ku -condense plan zake za muzik ili kufit ndani ya pindi kifupi cha uhai kilichabakia maana alijua hana muda mrefu wa kuishi, jimmy cliff msanii mwenzake anasema, bob alikua anakunywa chai na kula lunch kwapamoja asubuhi na kwenda mazoezi ya muziki siku nzima na hata usiku wa manane, ili kurekodi kila alichotaka kusema kwa njia ya nyimbo, hivyo jimmy cliff anaamini kwa kipindi hicho kifupi bob aliimba na kurekodi kila ujumbe aliotaka kufundisha kabla hajafa.

Pia moja ya madaktari waliokua wanamtibu bob alishangazwa na style yake ya uimbaji na ushikaji wake wa guiter (kama SMG) katika concert yake ya mwisho, hasa jinsi bob alivoimba wimbo wa REDEMPTION SONG,

"....these songs of freedom is all I ever had"

Daktari huyo alihisi maumivu makali (kutokana na kansa) aliyokua nayo bob kwa jinsi alivyokua akishika paji la uso mara kwa mara, baadae daktari huyo alikiri kwamba bob aliandaa concert hiyo maalum kwaajiri ya kuwaaga rasmi washabiki wake na kusisitiza mambo ya msingi ya kisiasa, kwani afya yake haikuruhusu kabisa.

Bob na timu yake walipokua kwenye mechi ya kirafiki kule ufaransa sote twajua aliumia kidoleni na kansa ikaanzia hapo, high times la endelea kuripoti kwamba kidole kile alicho umia ndicho kilicho chomwa na waya uliokua kwenye viatu, na mbaya zaidi akiwa uwanjani kuna daktari asiyefahamika alikuja kumchoma bob sindano (isiyofahamika) kwenye hicho kidole kama tiba. Lakini sindano hiyo inaripowa kuwa ilikua na lengo la kueneza viini vya kansa mwilini mwa bob. Kwa kweli nashindwa kuamini kama kweli CIA walimuua bob makusudi, sijui wadau mnalionaje hili.

By Fedor

Comments

Popular posts from this blog

NINI MAANA KIGOLI?. AU BINTI KIGOLI

Mambo 10, ya kumfanya mpenzi wako akupende milele@ Kama uliamini mapenzi pesa... SAHAU