Ureno yatinga fainali kwa kuindoa Wales
Ureno imekuwa nchi ya kwanza kuingia fainali ya michuano ya Euro baada ya kuzima ndoto za Wales kwa kuichapa magoli 2 - 0 katika mechi ya nusu fainali mjini Lyon nchini Ufaransa.
Mshambuliaji wa Ureno Cristiano Ronaldo ameendelea kuwa mwiba kwa wapinzani kwenye mashindano hayo baada ya kupachika goli kabla mshambuliaji wa zamani Manchester United Luis Nani kupigilia msumari wa moto kwenye kidonda kwa kupachika goli la pili.
Kwa matokeo hayo Ureno sasa itakutana na mwenyeji Ufaransa au Ujerumani katika mechi ya fainali.
Comments
Post a Comment