Gonzalez mwenye umbo refu, ataanza rasmi majaribio yake mara baada ya kikosi cha Azam FC kuanza mazoezi ya maandalizi ya msimu mpya
Klabu ya Azam FC, imempokea kipa, Juan Jesus Gonzalez, raia wa Hispania kwa ajili ya kufanya majaribio ya kujiunga na klabu hiyo itakayoshiriki michuano ya Kombe la Shirikisho 2017.
Kwa mujibu wa mtandao wa Azam ujio wa kipa huyo unatokana na benchi jipya la ufundi la Azam FC chini ya kocha Zeben Hernandez, ambalo linataka kuongeza nguvu kwenye eneo la langoni ili kutengeneza safu bora ya ulinzi na ushindani wa namba katika nafasi hiyo.
Gonzalez mwenye umbo refu, ataanza rasmi majaribio yake mara baada ya kikosi cha Azam FC kuanza mazoezi ya maandalizi ya msimu mpya (2016-17) Alhamisi.
“Nimefurahi sana kufanikiwa kwake kutua hapa, namjua Gonzalez ni kipa mzuri na hili ni jambo muhimu sana kwa Azam FC katika kuboresha eneo hilo, atakuwa hapa kwa majaribio akifanya vizuri tutamchukua,” amesema Zeben.
Comments
Post a Comment