Uchunguzi wafanywa Louisiana
Idara ya Sheria ya Marekani imefungua uchunguzi dhidi shambulizi baya la risasi lililofanywa na polisi dhidi ya mtu mwesi aliyekuwa akiishi katika kitongoji cha Baton Rouge katika mjini Louisiana.
Kufuatia tukio hilo la mauaji familia ya mwanaume huyo, Alton Sterling,imetoa wito kwa viongozi wa juu wa polisi kujiuzulu, na pia kumekuwa na maandamano kadhaa kufuatia kifo cha Alton na kufuatiwa na ujumbe wenye hasira kwenye mitandao ya kijamii baada ya video iliyowaonesha polisi wawili weupe waliokuwa wamemkandamiza chini bwana Sterling na kumpiga risasi hadi kufa siku usiku wa Jumanne .
Alton aliyekuwa na umri wa miaka thelathini na saba wakati huo baba mwenye familia alikuwa akichuuza santuri nje ya duka moja ,nao uchunguzi wa kitabibu unaonesha kwamba Alton alikufa kutokana na majeraha ya risasi zilizomuingia kifuani na kutokea upande wa nyuma
Comments
Post a Comment