Mwanamuziki Mr Blue Ataja Idadi ya Nyumba Anazomilika Hapa Bongo

Kama unadhani Mr Blue ni miongoni mwa wale wasanii wanaoishia kuwa maarufu tu lakini maisha yao yakiwa bado ‘msegemnege’ upo wrong.

Rapper huyo amesema kuwa hadi sasa ana nyumba tatu na zote zimetokana na muziki.

“Moja naishi, mbili zingine ndio ambazo najaribu kumaliziamalizia,” Blue alikiambia kipindi cha The Playlist cha Times FM Jumamosi iliyopita.

Hata hivyo Blue anasema kama angekuwa na akili hizo za maisha tangu miaka ya nyuma kwa sasa angekuwa na mali nyingi za kutisha lakini ujana na matumizi ya vilevi vilimponza.

Comments

Popular posts from this blog

NINI MAANA KIGOLI?. AU BINTI KIGOLI

Mambo 10, ya kumfanya mpenzi wako akupende milele@ Kama uliamini mapenzi pesa... SAHAU